Monday, 6 April 2015

KUDUMU KATIKA KUMWAMINI MUNGU WAKATI UNA TATIZO LA KIFEDHA




KUDUMU KATIKA KUMWAMINI MUNGU WAKATI UNA TATIZO LA KIFEDHA.......

  Nawasalimu katika jina la Bwana Yesu kristo..Ni wasaa mzuri tena napata kibali mbele zake na kujumuika nanyi katika kutangaza neno lake kama tulivyoamriwa tunasoma kitabu cha Mathayo 28:20...''na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaarumu ninyi''...Katika masomo yaliyopita nina imani kwa jina la Yesu kristo umeongeza kitu katika ufahamu wako. Kuna  mahala Mungu amekukusudia kufika katika jina la Yesu kristo..Barikiwa wewe ambaye umeamua kuchukua uamuzi mzuri wa kujifunza pamoja nami...
Ndugu mpendwa katika Bwana tutajifunza somo lenye kichwa cha habari.."KUDUMU KATIKA KUMWAMINI MUNGU WAKATI UNA TATIZO LA KIFEDHA..'' Katika maisha yetu ya kila siku fedha imechukua nafasi kubwa sana....kila kitu tukifanyacho kinahitaji fedha..Si Elimu,Ujenzi,Injili,n.k. Fedha hizi pia mbali ya kuwa muhimu pia ni changamoto kuzipata na katika familia fulani fulani zimekuwa ni kama ndoto..Hebu ndugu mpendwa tujiulize swali hili lenye changamoto ya kibinadamu...Mahusiano yako na Mungu yapoje wakati una tatizo la kifedha? Je? unadumu katika yeye au unamkosea na kutenda dhambi...Ukiwa unatafakari nafasi yako katika jibu hili..ningependa tushiriki kwa pamoja kusoma hadithi ya mjane mmoja katika Biblia katika kitabu kile cha 2 Wafalme 4:1-7....

''Basi,mwanamke mmoja miongoni mwa wake za wana wa manabii alimlilia Elisha,akasema,Mtumishi wako mume wangu amekufa; nawe unajua ya kuwa mtumishi wako alikuwa mcha BWANA; na aliyemwia amekuja ili ajitwalie wana wangu wawili kuwa watumwa. Elisha akamwambia,Nikufanyie nini? Niambie; una kitu gani nyumbani? Akasema, Mimi mjakazi wako sina kitu nyumbani,ila chupa ya mafuta. Akasema,Nenda,ukatake vyombo huko nje kwa jirani zako wote,vyombo vitupu;wala usitake vichache. Kisha uingie ndani,ukajifungie mlango wewe na wanao,ikavimiminie mafuta vyombo vile vyote; navyo vilivyojaa uvitenge. Basi akamwacha,akajifungia mlango yeye na wanawe; hao wakamletea vile vyombo,na yeye akamimina. Ikawa,vilipokwisha kujaa vile vyombo,akamwambia mwanawe,Niletee tena chombo. Akamwambia,Hakuna tena chombo. Mafuta yakakoma. Ndipo akaja akamwambia yule mtu wa Mungu. Naye akasema,Enenda ukayauze mafuta haya,uilipe deni yako;nayo yaliyosalia uyatumie wewe na watoto wako..'' 
   Ndugu mpendwa katika kristo,baada ya kusoma kisa hiki cha mama huyu mjane kuna kitu hapa tutakwenda kujifunza..Zingatia hili ndugu yangu mpendwa, Mungu atabaki kuwa Mungu hata kama hajajibu jinsi wewe unavyotaka..ni lazima tuchunge mahusiano yetu na Mungu katika kila aina ya changamoto tunazopitia. Changamoto ya kifedha isikufanye ukapokea rushwa katika kazi yako..isikufanye ukapoteza uthamani wako kwa Mungu maana wewe ni wa dhamani..ooh haleluyaaa!!
Haya ni baadhi ya mambo kadhaa ambayo yatakusaidia uweze kudumu katika uhusiano na Mungu hata kama upo na changamoto za kifedha;
  • Tafuta msaada toka kwa Mungu kwanza: 
Katika hali ya kibinadamu ni kawaida kabisa kuwako hali ya kuchanganyikiwa endapo umepatwa na jambo fulani liwe tatizo au changamoto..wengi wetu huwa tunajitahidi sana kutafuta suluhisho kutoka kwa ndugu,jamaa na marafiki na wakati mwingine kukwama kabisa na wengine wasio na nguvu ya kustahimili kuishia hata kujiua..Ashukuriwe Mungu maana kuanzia leo hii hutajiua wala hutokata tamaa tena katika jina la Yesu kristo...
Mama huyu mjane ananibariki sana mana mbali na deni alokuwa nalo kumbuka alimpoteza pia mumewe..katika hali hiyo ni Mungu pekee ndo anaweza kuwa na msaada wa kweli...alichokifanya mama huyu alitafuta msaada toka kwa Mungu kwa kupitia mtumishi wake Elisha..mana alikuwa anadaiwa deni ambalo aliliacha mumewe na mdai alitaka fedha yake na kumbuka aliwataka watoto kulipia deni ile..mama huyu alitambua hana msaada mwingine zaidi ya kumkimbilia Elisha ambaye mumewe alikuwa mtumishi wake..ni kwa watumishi wa Mungu pekee ndipo tunapopata msaada. Kuna mambo mengine hayawezi kutatulika kibinadamu ni mpaka Mungu ahusishwe...

  • Kuwa mtiifu mbele za Mungu
Ndugu mpendwa katika Bwana utiifu mbele za Mungu ni kitu cha thamani sana..kutii kwako kunaweza kukawa mpenyo wa jambo lililokuwa linakutatiza muda mrefu,jawabu la maswali mengi ulokuwa ukijiuliza pasipo majibu..''Kutii kunaleta mpenyo'(Breakthrough)..Tunasoma katika kifungu chetu kile  cha 2Fal 4:2-4..Katika kifungu hiki utaona mtumishi wa Mungu Elisha alimwuliza mama yule mjane Nikufanyie nini? tena akasema, una kitu gani nyumbani? mama yule mjane ''akasema mimi mjakazi wako sina kitu nyumbani,ila chupa ya mafuta'' Baada ya hapa ndipo kutoboza kwa huyu mama kulipoanzia mana alitii maelekezo yote ya Mtumishi wa Mungu Elisha...swali la kujiuliza JE? ni mara ngapi wewe unapewa maelezo na mchungaji wako/kiongozi wako unafuata? Wengi wetu huwa tunapuuzia,wakati mwingine tunaitika bila kuyafanyia kazi..kwa jinsi hiyo huwa tunapishana na msaada kutoka kwa Mungu kwa sababu ya kutokutii kwetu..'Mungu akakupe utiifu kuanzia leo katika jina la Yesu kristo....
Baada ya kufanya kama alivyo agizwa hatimaye chupa zote zilijaa mafuta..biblia inaniambia mama huyu mjane alirudi kwa mtumishi wa Mungu Elisha kupata maelezo mengine hii inaonyesha jinsi gani mama huyu alizidi kutii mamalaka ya Kiungu..JE? ingalikuwa wewe ungerudi kwa Mtumishi wa Mungu Elisha?

  • Endeleza uhusiano na Mungu
Katika kifungu hiki 2Fal 4:7..''ndipo akaja akamwambia yule mtu wa Mungu. Naye akasema,Enenda ukayauze mafuta haya,uilipe deni yako;nayo yaliyosalia uyatumie wewe na watoto wako...
Hebu tazama mama huyu alivyokuwa na hekima ya Mungu..alikuwa na subira baaada ya vyombo kujaa,hakuwa na papara alirudi kwa Mtumishi wa Mungu Elisha kwa maelekezo zaidi..aliendeleza,alidumisha uhusiano wake na mtumishi wa Mungu..JE? ni mara ngapi wewe unafanya pasipo maelekezo ya watumishi wa Mungu? ungalikuwa ni huyu mama ungerudi kwa Elisha? Mama huyu alitambua uhusiano na Elisha ni muhimu sana kwa saa ile mana alikuwa hajui ni nini cha kufanya na yale mafuta katika vyombo vyote vile? Ndugu mpendwa kuna mamlaka ya kiungu hapa nataka uone...na mama huyu alitambua na ndo mana alirudi kwa mtumishi. Neno moja tu la kimamlaka litakupa upenyo katika maisha yako ukiwa katika mahusiano mazuri na Mungu katika hali ngumu ya kifedha kama mama huyu mjane..''Enenda ukayauze mafuta haya''.......maneno haya ya Elisha yaliambatana na mamlaka ya Kiungu ndani yake..taka yasitake mafuta yangeuzika tu kwa sababu nabii wa Bwana ametamka katika jina la Yesu kristo.....

  • Kila kitu kinaanzia nyumbani
Ndugu mpendwa hivi unafahamu baraka,ustawi,kutoboza kwako kunaanzia nyumbani? Hebu tujikumbushe tena mstari huu kuhusu mama yule mjane..''Nikufanyie nini? Niambie; una kitu gani nyumbani?...oooh haleluya...Kumbe huwezi kufanikiwa pasipokuwa na kitu nyumbani..''AKIBA'' Mama huyu mjane alikuwa na chupa ya mafuta,WEWE una nini? Mungu apate kukubariki? apate kukutoa hapo ulipo? apate kutibu ndoa yako? apate kufuta deni zako zote? Hebu tujadili mfano huu...Ukitaka kukopa fedha 'Bank' unaulizwa swali rahisi tu, Una dhamana gani? mana yake; Una akiba? Una chupa ya mafuta? Ni vizuri kuanzia hapa sasa tuanze kujiwekea chupa ya mafuta nyumbani hata siku mdeni wetu akija kuchukua chake tuwe na mafuta ya kujiuzia baadae katika jina la Yesu kristo....Kumbuka ni chupa ya mafuta pekee(AKIBA) ndiyo iliyomtoa mama yule mjane katika kufanywa wanawe watumwa...

                                                  ************AMEN***********

No comments:

Post a Comment