Tuesday, 17 March 2015

MAISHA NI JUKUMU LA MUDA MFUPI...


MAISHA NI JUKUMU LA MUDA MFUPI-1

Nawasalimu katika jina la bwana wetu Yesu kristo. Napenda kutanguliza shukrani zangu za pekee kwa Muumba wetu na kwa mpendwa mwanaye wa pekee ( Yesu kristo) kwa kunipa KIBALI hiki cha kushiriki katika neno lake takatifu.

Leo nina furaha iliyo kuu sana na ya kipekee kushiriki pamoja nanyi katika mafundisho haya mafupi ya  neno lake..Kabla sijaanza mafundisho ya neno letu la siku ya leo ambalo lina kichwa cha habari "MAISHA NI JUKUMU LA MUDA MFUPI" ningependa utambue na kukumbuka kuwa ndani ya 'NENO' ndimo kuliko na uzima..tunasoma katika kitabu cha Yoh 1:1-4..Hapo mwanzo palikuwako neno,naye neno alikuwako kwa Mungu.....

Naamini kabisa ndani ya neno hili ndimo uzima ulipo na uzima huu utakuwa nuru ndani ya maisha yako na wala giza halitakuweza kamwe. Ningependa uelewe kitu hapa ukiwa umeshiba neno au neno la Mungu limejaa ndani yako hakuna nguvu zozote za giza zitakazo kuweza..Yoh 1:5..nayo nuru itang'aa gizani,wala giza halikuiweza..ndugu mpendwa giza ni shida za kuzimu,magojwa,umasikini...neno likijaa ndani yako haya yote hayata kupata kwamwe katika jina la Yesu kristo.
.............................................................................
Tumesha elewa sasa kuwa neno ni uzima na ni nuru pia sasa naamini kabisa katika jina la Yesu kuwa somo letu la leo linakuwa uzima na nuru kwako maishani katika jina la Yesu kristo.
Somo letu la leo la MAISHA NI JUKUMU LA MUDA MFUPI,biblia imeelezea mifano mingi kupitia Wafalme na Manabii wake kuwa ni jinsi gani maisha yetu duniani yalivyo mafupi na yasiyodumu.
(mafupi-si ya umilele,yasiyodumu-ni makazi ya muda tu hivyo hatupaswi kujishikanisha nayo).
Tunasoma katika Zab 119:19..Mimi ni mgeni katika nchi,usinifiche maagizo yako. Ndugu yangu mpendwa mwimbaji zaburi anasema yeye ni mgeni katika nchi..hii ina maana kuwa hakuwa wa kudumu katika nchi ile alikuwa anapita tu ni kama alipewa hifadhi ya muda tu,ni kama alikuwa safarini kuelekea mahala fulani,ni kama safari yake haijakoma bado..ukiwa mgeni mahali una muda wa kukaa hapo na lazima uwe na kibali au ruhusa ya kuwa mahali hapo maana hapo si pako,si makazi yako unapita tu..Mfano: Umesafiri nchi ya ugeni ni lazima uwe na kibali cha kuishi pale na lazima kionyeshe ni muda gani utakuwa hapo na muda ukisha kwisha utarudi ulipo toka...ndivyo yalivyo maisha ya kiroho duniani si makazi yetu ya milele ni pa muda tu umilele wetu upo mbinguni..hivyo hatupaswi kujishikiza na vya dunia hii maana ni vya muda tu...tunasoma kitabu cha Ebr 11:13-16...hawa wote wakafa katika imani,wasijazipokea zile ahadi,bali wakaziona tokea mbali na kuzishangilia,na kukiri kwamba walikuwa wageni na wasafiri juu ya nchi......

Jambo la kuzingatia na muhimu ni kutambua kuwa kitambulisho chetu kiko katika umilele na nchi yako ni mbinguni..tunapofahamu ukweli huu tutaacha kuwa na wasiwasi wa kupata kila kitu katika dunia hii ambayo mimi na wewe ni wapangaji ndani yake.
Ningependa ushiriki nami katika kumuomba Mungu akusaidie kutambua jinsi ya muda wa kukaa hapa duniani ulivyo mfupi.....
AMEN...







2 comments: