Friday, 20 March 2015

MAISHA NI JUKUMU LA MUDA MFUPI-2

    Ndugu wapendwa nawasalimu katika jina la Yesu kristo..Napenda kuchukua nafasi hii ya kitumishi kushiriki nanyi tena katika mwendelezo wa neno letu 'MAISHA NI JUKUMU LA MUDA MFUPI'' kadiri ya mwongozo wa Roho mtakatifu..Ni tumaini langu pia, utakuwa umeshiriki katika kumuomba Mungu akusaidie kutambua na kuyaona maisha ya hapa duniani kwa mtazamo tofauti...kumbuka katika sehemu iliyopita tuliona jinsi manabii wa zamani walivyojinyeyekesha mbele ya Mungu wetu na kumwomba awasaidie kuyaona maisha ya duniani kama ayaonavyo yeye (si yakudumu)..
Tunasoma katika biblia kitabu cha Ayubu 8:9..kwani sisi tu wa jaha tu,wala hatujui neno,kwa kuwa siku zetu duniani ni kivuli tu,,
   Mtumishi wa Mungu Ayubu' anazidi kutupa uhakika katika kile kitabu chake kuwa ni jinsi gani maisha ya hapa duniani yalivyo mafupi si ya kudumu tena yeye anasema kuishi kwetu hapa duniani,siku zetu ni kama kivuli tu...kwa maana hazihesabiki...Hebu tuzidi kutazama katika vitabu vingine ndani ya biblia yetu tukufu jinsi watumishi wengine mbali na Mtumishi wa Mungu Ayubu aonavyo maisha ya hapa duniani yalivyo mafupi...
   Tusome Ebr 13:4...maana hapa hatuna mji udumuo,bali twautafuta ule ujao. Katika mstari huu biblia inazidi kutuhakikishia kuwa hapa duniani si makazi ya kudumu ipo sehemu ambayo sisi ndipo tunastahili hasa kuwapo milele napo ni Mbinguni katika jina ya Yesu kristo!!!!!! Hebu tuone nini mwimba zaburi anatuambia juu ya hili tusome..Zab 39:12..Ee bwana, usikie maombi yangu,utege sikio lako niliapo,usiyanyamalie machozi yangu..kwa maana mimi ni mgeni wako,msafiri kama baba zangu wote...

    Mtunga zaburi anazidi kutufunulia kuwa mbali na kuwa wageni bali pia ni wasafiri akimaanisha tunapita hapa duniani kuna mahala tunaelekea ambapo ndipo tunastahili sisi kuwapo kama jinsi baba zake walivyokuwa wasafiri..wacha tuone tena katika kitabu cha Wakoritho kinasemaje kuhusu uhalali wetu hapa duniani je? ni wa kudumu au la...tunasoma 1Kor 7:31..Na wale wautumiao ulimwengu huu,kama hawautumii sana,kwa maana mambo ya ulimwengu huu yanapita...tunazidi kusoma mistari mbalimbali katika vitabu mbalimbali vikituonyesha na kutuhakikishia kuwa mahala hapa si petu mambo ya hapa yote yanapita..hatupaswi kushikamana nayo mpaka tumsahau Mungu..na kumbuka Mungu ametuweka tu waangalizi mali zote na vyote vilivyomo ni vyake..tunasoma.. Zab 24:1..Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya BWANA..Dunia na wote wakaao ndani yake...hivyo yapaswa kutambua hakuna uhalali wa umiliki wowote mana sisi ni wapangaji...nyumba,fedha,magari,wanyama vyote ni vyake na sisi ni waangalizi tu..!!!!!!
Hebu tutazame tena kitabu cha 2Kor 4:18...tusiviangalie vinavyoonekana,bali visivyoonekana. Kwa maana vinavyoonekana ni vya muda tu; bali visivyoonekana ni vya milele...kumbe vinavyoonekana ni vya muda tu..magari,fedha,dhahabu bali uweza wa Mungu,mamlaka yake,nguvu zake ni za milele mana hivyo huwezi kuviona katika macho haya ya damu na nyama bali ya rohoni na ndo umilele wenyewe katika jina la Yesu kristo aliye hai!!!!! na umilele huu unapatikana mbinguni ambapo ndipo makazi yetu ya milele..oooh haleluya!!!!
   Hebu tumalizie sehemu yetu ya somo kwa kutazama tena kitabu cha Efe 2:19...Basi tangu sasa ninyi si wageni wala wapitaji,bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu,watu wa nyumbani mwake Mungu....ndugu msomaji wa neno hili ni katika kitabu hiki tu (Efeso) Mungu ametupa hakikisho la sisi kutokuwa wageni bali wenyeji..Kumbuka hauwezi kuwa mwenyeji kama hutafanya mapenzi yake,hutamzalia matunda,hutazifuata za kuzishika amri zake na yote haya tutayapata kwa kumsikiliza yeye aliyetumwa na yeye ambaye amefanyika dhambi ili sisi tupate patanisho na hakikisho la umilele ( yaani tusiwe wageni tena katika jina la Yesu Kristo!!!!!!!!!!

************************************AMEN*****************************

    


Tuesday, 17 March 2015

MAISHA NI JUKUMU LA MUDA MFUPI...


MAISHA NI JUKUMU LA MUDA MFUPI-1

Nawasalimu katika jina la bwana wetu Yesu kristo. Napenda kutanguliza shukrani zangu za pekee kwa Muumba wetu na kwa mpendwa mwanaye wa pekee ( Yesu kristo) kwa kunipa KIBALI hiki cha kushiriki katika neno lake takatifu.

Leo nina furaha iliyo kuu sana na ya kipekee kushiriki pamoja nanyi katika mafundisho haya mafupi ya  neno lake..Kabla sijaanza mafundisho ya neno letu la siku ya leo ambalo lina kichwa cha habari "MAISHA NI JUKUMU LA MUDA MFUPI" ningependa utambue na kukumbuka kuwa ndani ya 'NENO' ndimo kuliko na uzima..tunasoma katika kitabu cha Yoh 1:1-4..Hapo mwanzo palikuwako neno,naye neno alikuwako kwa Mungu.....

Naamini kabisa ndani ya neno hili ndimo uzima ulipo na uzima huu utakuwa nuru ndani ya maisha yako na wala giza halitakuweza kamwe. Ningependa uelewe kitu hapa ukiwa umeshiba neno au neno la Mungu limejaa ndani yako hakuna nguvu zozote za giza zitakazo kuweza..Yoh 1:5..nayo nuru itang'aa gizani,wala giza halikuiweza..ndugu mpendwa giza ni shida za kuzimu,magojwa,umasikini...neno likijaa ndani yako haya yote hayata kupata kwamwe katika jina la Yesu kristo.
.............................................................................
Tumesha elewa sasa kuwa neno ni uzima na ni nuru pia sasa naamini kabisa katika jina la Yesu kuwa somo letu la leo linakuwa uzima na nuru kwako maishani katika jina la Yesu kristo.
Somo letu la leo la MAISHA NI JUKUMU LA MUDA MFUPI,biblia imeelezea mifano mingi kupitia Wafalme na Manabii wake kuwa ni jinsi gani maisha yetu duniani yalivyo mafupi na yasiyodumu.
(mafupi-si ya umilele,yasiyodumu-ni makazi ya muda tu hivyo hatupaswi kujishikanisha nayo).
Tunasoma katika Zab 119:19..Mimi ni mgeni katika nchi,usinifiche maagizo yako. Ndugu yangu mpendwa mwimbaji zaburi anasema yeye ni mgeni katika nchi..hii ina maana kuwa hakuwa wa kudumu katika nchi ile alikuwa anapita tu ni kama alipewa hifadhi ya muda tu,ni kama alikuwa safarini kuelekea mahala fulani,ni kama safari yake haijakoma bado..ukiwa mgeni mahali una muda wa kukaa hapo na lazima uwe na kibali au ruhusa ya kuwa mahali hapo maana hapo si pako,si makazi yako unapita tu..Mfano: Umesafiri nchi ya ugeni ni lazima uwe na kibali cha kuishi pale na lazima kionyeshe ni muda gani utakuwa hapo na muda ukisha kwisha utarudi ulipo toka...ndivyo yalivyo maisha ya kiroho duniani si makazi yetu ya milele ni pa muda tu umilele wetu upo mbinguni..hivyo hatupaswi kujishikiza na vya dunia hii maana ni vya muda tu...tunasoma kitabu cha Ebr 11:13-16...hawa wote wakafa katika imani,wasijazipokea zile ahadi,bali wakaziona tokea mbali na kuzishangilia,na kukiri kwamba walikuwa wageni na wasafiri juu ya nchi......

Jambo la kuzingatia na muhimu ni kutambua kuwa kitambulisho chetu kiko katika umilele na nchi yako ni mbinguni..tunapofahamu ukweli huu tutaacha kuwa na wasiwasi wa kupata kila kitu katika dunia hii ambayo mimi na wewe ni wapangaji ndani yake.
Ningependa ushiriki nami katika kumuomba Mungu akusaidie kutambua jinsi ya muda wa kukaa hapa duniani ulivyo mfupi.....
AMEN...